Kuna ulazima kwa Shirikisho la soka nchini (TFF) kupitia kwa Kamati yake ya Waamuzi kuangalia namna ya kuwasaidia waamuzi wanaochezesha ligi kuzifahamu vyema baadhi ya sheria za mchezo wa soka hasa sheria ya kuotea.
Kumekuwa na makosa mengi sana ambayo yamekuwa yakiainishwa kutoka michezo mbalimbali msimu huu kuonyesha jinsi waamuzi wasaidizi wanavyoboronga kutambua matukio ya kuotea.
Kwenye mchezo wa jana kati ya Yanga dhidi ya Lipuli Fc uamuzi wa kuotea uliotolewa kwa Mrisho Ngasa kwenye dakika ya 52 uliwashangaza wengi.
Picha za marudio ya runinga ya Azam zinaonyesha dhahiri kuwa Ngasa aliondoka wakati sahihi kuuwahi mpira wa juu uliopigwa na Kelvin Yondani na kuivuka safu ya ulinzi ya Lipuli.

Kama tukio lile lisingeamuliwa kuwa offside, Yanga ingeweza kufunga bao la pili.
Kimsingi yalikuwa ni maamuzi ya hovyo na hakika ni aibu kwa waamuzi wetu kuendelea kufanya makosa hayo licha ya kulaumiwa na kuadhibiwa mara kwa mara.
Hii inaonyesha wengi hawafahamu tafsiri sahihi ya mchezaji kuotea. Wanadhani mchezaji akibaki peke yake na mlinda lango (bila ya kujali mazingira yaliyopelekea hali hiyo) basi ameotea.

ADVERTISE HERE