Chipukizi Maka Edward aliyepandishwa kutoka kikosi cha pili cha Yanga (Yanga B) ameendelea kudhihirisha kuwa ni mmoja wa viungo mahiri, turufu kwa klabu ya Yanga.
Maka alianza kukitumikia kikosi cha kwanza cha Yanga wakati wa michuano ya SportPesa na kiwango chake kilizivutia timu mbalimbali ikiwemo Azam FC iliyojaribu kumsajili bila mafanikio.
Kwenye kikosi cha Yanga Maka amekabidhiwa jezi namba nane iliyokuwa inavaliwa na kiungo aliyetimkia Simba Haruna Niyonzima.
Maka amekuwa akimudu vyema nafasi ya kiungo na amedhihirisha hilo kila anapopewa nafasi na Mwalimu.
Kutokana na Yanga kukabiliwa na michuano mingi ni dhahiri kocha George Lwandamina ataendelea kumpa nafasi kwenye kikosi chake ili aimarike zaidi.
Amecheza michezo yote ya kirafiki ya Yanga.
Mbali na Maka wachezaji wengine waliopandishwa kutoka Yanga B ni Yusuph Mhilu na Said Mussa.

ADVERTISE HERE