Yanga imeendeleza wimbi la ushindi kwenye uwanja wa Taifa baada ya leo kuichapa Lipuli Fc kwa bao 1-0.
Huo ni ushindi wa nane kutoka michezo tisa iliyopigwa dimba la Taifa.
Yanga iliyoanza mchezo huo kwa kasi ilijipatia bao lake la ushindi kwenye dakika ya 10 mfungaji akiwa Heritier Makambo aliyemalizia pasi murua ya Mrisho Ngasa.
Hilo ni bao la nne kwa Makqmbo katika ligi msimu huu

Takwimu za mchezo huo zinaonyesha Yanga ilitawala kwa muda mwingi huku ikitengeneza nafasi nyingi zaidi kuliko wapinzani wao.

Yanga ilimaliza mchezo huo ikiwa na wachezaji 10 uwanjani baada ya kinda Paulo Godfrey kuonyeshwa kadi ya pili ya njano wakati mchezo huo unaelekea ukingoni.
Matokeo hayo yameirejesha Yanga kwenye nafasi ya pili baada ya kufikisha alama 25 ikiipiku SImba yenye alama 23.
Azam Fc iko kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia alama 27.
Azam imecheza michezo miwili zaidi ya Yanga.

ADVERTISE HERE