Beki wa zamani wa Simba, Jamali Mwambeleko ambaye alisaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia klabu hiyo amekiri kuwa alizingua mwenyewe kwa kukataa kujiunga na Yanga.
Mwambeleko alisajiliwa na Simba akitokea katika klabu ya Mbao mwanzo wa msimu huu aliomba barua ya kuvunjwa kwa mkataba wake kwa kuwa alikuwa hapati nafasi ya kucheza ili ajiunge na Singida United.
Hivi karibuni Mwambeleko amesajiliwa na klabu ya KCB ya Kenya baada ya kuvunja mkataba wake na Singida United iliyoshindwa kumlipa mshahara kwa miezi miwili.
Mwambeleko anasema kabla ya kusaini Simba viongozi wa Yanga walimfuata na kutaka asaini mkataba katika klabu yao.
“Nilishindwa kukubaliana nao kwa kwani walikuja mali kauli, lakini Simba walikuja na pesa mkononi ndio maana nikakubali kwenda kusaini,” alisema.
“Baadae nilikuja kuona kwamba nimezingua na huenda sikufanya uamuzi sahihi kwani kocha wa Yanga, George Lwandamina ndio alikuwa akinitaka zaidi kwa wakati huo.
“Huenda kutokufanya uamuzi sahihi zaidi lakini, Lwandamina hata alipoondoka nchini nilikuwa nikiwasiliana naye na kuniambia akipata timu Zambia yenye mahitaji ya mchezaji kama mimi ataniita, “ alisema Mwambeleko.
“Hata hapa KCB mkataba wangu upo wazi kama naweza kupata timu nyingine kabla ya mkataba kumalizika wanaweza kuniuza na hicho kilichangia nisisaini mkataba Gor Mahia kwani nao walikuwa wananihitaji kabla ya kuja hapa KCB, “ aliongezea.
Mwambeleko baada ya kupata barua hiyo kama mchezaji huru alitimkia Singida United ambapo alisaini mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Sh 15 milioni.
Mwambeleko alikaa hapo Singida ndani ya mwezi mmoja tu akicheza mechi mbili dhidi ya Biashara United na African Lyon na aliondoka katika klabu hiyo kwa madai walishindwa kumtimizia mahitaji yaliyokuwa katika mkataba wake.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE