Uongozi wa Yanga umethibitisha kuwa kiungo wake kinara wa kutengeneza nafasi za mabao Ibrahim Ajib bado anasumbuliwa na maumivu ya mgongo hivyo ataukosa mchezo wa kesho dhidi ya Lipuli Fc.
Pia Mcongo Papi Tshishimbi ambaye pia alikosa mchezo uliopita dhidi ya KMC, atakosekana tena.
Hata hivyo licha ya kukosekana kwa wachezaji hao muhimu, Yanga bado ina kikosi imara kinachoweza kuondoka na alama zote tatu uwanja wa Taifa kesho Jumanne.
Katika mchezo dhidi ya KMC Yanga haikuwa na wachezaji hao na iliweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0 ingawa ililazimika kusubiri maajabu ya Fei Toto aliyefunga bao la ushindi kwenye dakika ya 90.
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera alisifu kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake licha ya kuwakosa wachezaji hao muhimu.
Huenda kesho Zahera atatumia kikosi kilekile kilichoilaza KMC siku ya Alhamisi.
Hata hivyo kukosekana kwa Ajib kunamlazimu Zahera abadili mfumo kwani Ajib ndiye anayehusika kutengeneza mabao mengi ya Yanga.
Kati ya mabao 15 yaliyofungwa, Ajib amefunga mabao matatu na kutengeneza nafasi za mabao nane.
Kiungo mkongwe Thabani Kamusoko alikabidhiwa majukumu ya Ajib kwenye mchezo dhidi ya KMC na huenda akaendelea na majukumu hayo kwenye mchezo wa kesho.

ADVERTISE HERE