Yanga leo imeendeleza rekodi ya kupata ushindi kwenye michezo yake ya kirafiki visiwani Zanzibar baada ya kuichapa Jamhuri ya Pemba bao 1-0 kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye dimba la Gombani kisiwani Pemba.
Bao pekee la Yanga lilifungwa na mlinzi wa pembeni Haji Mwinyi Mngwali kupitia mpira wa adhabu nje kidogo ya 18.
Huo unakuwa ushindi wa pili mfululizo na wa 1-0 pia katika kambi ya Yanga kisiwani Pemba kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu wa jadi, Simba Jumatano Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya Alhamisi kuifunga Chipukizi 1-0, bao pekee la Ibrahim Hajib.
Na kwa ujumla huo ni mchezo wa tatu kwa Yanga visiwani Zanzibar, baada ya Jumapili ya wiki iliyopita kuifunga Mlandege mabao 2-0 Uwanja wa Amaan, Zanzibar mabao ya Hajib na Mzimbabwe Donald Ngoma.
Kocha wa Yanga George Lwandamina leo alipanga vikosi viwili tofauti kila kipindi, lakini kile kilichoonekana kusheheni nyota wenye vipaji na uzoefu zaidi ndicho kiliishia kucheza soka ya kuvutia bila kufunga bao kipindi cha pili.
Ajib alikaribia kufunga bao la tatu mfululizo katika mechi tatu za Yanga baada ya kupiga juu ya lango dakika ya 88 kufuatia kazi nzuri ya kiungo Mzimbabwe, Thabani Kamusoko.
Aidha kiungo Papi Kabamba Tshishimbi amevaa uzi wa Yanga kwa mara ya kwanza leo, akiingia kwenye kipindi cha pili. Japo alionekana dimbani kwa muda mfupi lakini uwezo alio-onyesha sio wa kutia mashaka.

Vikosi vya Yanga SC leo vikulikuwa; kipindi cha kwanza; Ramadhani Kabwili, Juma Abdul, Mwinyi Mngwali, Abdallah Hajji ‘Ninja’, Nadir Haroub ‘Cannavaro’/Pato Ngonyani dk34, Maka Edward, Pius Buswita, Said Juma ‘Makapu’, Amissi Tambwe/Said Mussa dk34, Matheo Anthony na Juma Mahadhi/Yussuf Mhilu dk34.
Kipindi cha pili; Youthe Rostand, Hassan Kessy/Juma Abdul dk70, Gardiel Michael, Kevin Yondan, Andrew Vincent ‘Dante’, Papy Kabamba Tshisbimbi, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma, Ibrahim Ajib, Emanuel Martin na Raphael Daudi

ADVERTISE HERE