Kiungo wa Yanga, Feisal Salum 'Fei Toto' amesema ndoto yake kubwa katika soka ni kutaka kufikia anga alizofikia nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta.
Samatta kwa sasa anaichezea klabu ya Genk ya Ubelgiji baada ya kutamba na Simba na baadae TP Mazembe ya DR Congo.
Samatta amekuwa na msimu mzuri barani Ulaya na tayari ameanza kuhusishwa na baadhi ya timu zinazoshiriki ligi kuu ya Uingereza.
Fei Toto amebainisha kuwa ana ndoto ya kucheza nje ya nchi na mafanikio ya nahodha huyo wa Taifa Stars yanamfanya ajitume zaidi kwani anaamini hakuna jambo lisilowezekana.
Amesema anajituma ili kuweka kiwango chake cha sasa juu na hatimaye kutimiza ndoto yake hiyo.<
"Mimi binafsi natamani mafanikio ya Samatta, ametuonyesha njia na kwangu natamani kufikia alipofika yeye," Fei Toto amenukuliwa na gazeti la Nipashe
Amesema Yanga ni moja ya timu kubwa na kwake hiyo ataitumia kama ngazi ya kufika mbali.
"Hakuna mchezaji ambaye hapendi mafanikio makubwa, kucheza nje ya nchi ni moja ya ndoto zangu"
Kiungo huyo kutoka Zanzibar, aliifungia timu yake bao muhimu kwenye mchezo dhidi ya KMC ambao Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0.
Ushindi huo uliifanya Yanga kufikisha pointi 22 ikiizidi Simba inayoshika nafasi ya tatu kwa pointi mbili.
Kikosi hicho cha kocha Mwinyi Zahera kitashuka uwanjani keshokutwa Jumanne kuumana na Lipuli FC.

ADVERTISE HERE