Kwa kasi ya Yanga, mashabiki wake wana uhakika msimu huu wanarejesha taji lao kutoka kwa Simba, lakini Kocha Mwinyi Zahera amesema bado ni mapema sana.
Zahera amesema ni mapema kutabiri hilo kwa kuwa, ligi bado ngumu na mechi bado nyingi, lakini ameandaa jeshi lake kwa ajili ya kubeba ubingwa na hata wachezaji wanafahamu hilo.
“Tumecheza mechi nane mpaka sasa, tumeshinda zote na tuna sare moja, lakini ni mapema sana kutabiri ubingwa kwa sababu ligi bado ngumu.
"Lakini, tunataka ubingwa, tunataka kushinda kila mchezo na tutakabiliana na mazingira ama yeyote ambayo atakuja mbele yetu kutuzuia atapigwa tu,” alisema Zahera.
VIPI KWA AJIBU HAPO?
“Ndoto yangu kubwa kabla sijaondoka Yanga ni kumwona Ajibu akiwa tegemeo katika timu. Nataka kumwona Ajibu akiwa na majukumu kama ya Iniesta ama Xavi ama Mesut Ozil pale Arsenal.
"Ni mchezaji mweye akili kubwa ya mpira na ana mbinu nyingi, lakini bado hajafahamu hilo kwa undani. Najaribu kumweleza kila wakati, hastahili kucheza kwenye viwanja vya vumbi kwa sababu nafasi yake iko Ulaya sio hapa Tanzania.
“Namshukuru ameanza kunielewa kitu gani nataka afanye kwa faida ya klabu na yeye, akifika hapo ninapotaka mtaona umuhimu wake hadi Taifa Stars. Nataka Ajibu apandishe mashambulizi na kushuka kusaidia mabeki pindi mpira ukiwa kwa adui, hilo ndio soka la kisasa na hapo ndipo ataweza kuibeba timu na kuamua mechi kubwa,” anasema Zahera na kuongeza:
“Ajibu akifikia hatua hiyo nawaambia mtamsikia kwenye mitandao ya kimataifa kama Mbwana Samatta, hawezi kubaki Afrika, nipo tayari kupambana kumfikisha mbali zaidi na sitaacha kumkosoa pale anapokosea ili awe bora.”
AWACHAMBUA NGASSA NA KASEKE
Mawinga wake Mrisho Ngassa na Deus Kaseke wana staili tofauti ya uchazaji, hata pumzi wanatofautiana kwani mmoja ana kasi kuliko mwingine.
Hapa Zahera mwenyewe anasema, Kaseke ni zaidi ya Ngassa kwa kuwa anaweza kupanda kushambulia na kushuka kusaidia kukaba kwa wakati.
“Kaseke akipoteza mpira anashuka na adui kuutafuta, lakini Ngassa bado hana kasi kama hiyo licha ya kuwa anapambana vizuri japo wakati mwingine wanawapa mzigo mzito mabeki kupambana na washambuliaji pinzani kitu ambacho sio salama kwa timu.
KABWILI APIGIWA HESABU
“Ni mapema sana kumzungumzia huyu kijana amesharudi katika mstari na nimegundua ni mchezaji mzuri, namuandalia mazingira ya kumpa baadhi ya mechi ili kukua zaidi.
“Nataka kumkuza kama ilivyo kwa Paul Gordfey (Boxer) ambaye nadhani wengi hamkuwa mkimfahamu lakini, shughuli yake mnaweza kuwauliza washambuliaji wa Simba wanamjua.
“Hivyo Kabwili kuna siku mtamwona na kupigwa butwaa wenyewe akiwa amesimama pale langoni akipambana kuiokoa Yanga, namkubali sana lakini kila kitu kina muda wake.
“Hata Yohana Mkomola naye bado ana nafasi kubwa kikosini hapo, suala ni kuendelea kupambana mazoezi ili kuwa fiti zaidi,” anasema.
VIPI KAMBI PALE NEFALAND
Kama unadhani Yanga bado ina ukata kama zamani basi uko nyuma sana na matukio, Nefaland ilipo kambi ya Yanga wanakula bata kinoma.
Wafanyakazi na mabosi wa hoteli ya Nefaland mahaba kwa Yanga ni kama yoteee unaambiwa.
Wahudumu wanapata mzuka kinoma kutoka kwa Zahera na wachezaji wake na wanafurahia uwepo wa kikosi hicho.
Meneja wa hoteli hiyo Magreth Kilonzo, anasema wachezaji wa Yanga wamekuwa na nidhamu ya hali ya juu wanapokuwa kambi hapo.
“Tunaishi vizuri sana na kila mfanyakazi ana furaha kuwaona Yanga wapo hapa. Wanafurahi na kuzungumza nasi tofauti na watu wanavyowaona kwenye TV, wana nidhamu na ni wastaarabu sana.
“Kuna baadhi ya wachezaji wana majina makubwa na tupo nao hapa, tunazungumza na kucheka. Uongozi unalipa bili zetu kwa wakati, hakuna usumbufu hata kidogo,” anasema meneja huyo.
Makala hii ni kwa hisani ya gazeti la Mwanaspoti

ADVERTISE HERE