Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema suala la kusajiliwa kwa mshambuliaji raia wa Zambia Obrey Chirwa limefungwa rasmi.
Zahera amesema leo katika kambi ta timu hiyo kwamba hataweza kumchukua Chirwa kufuatia Nidhamu ndogo ya mshambuliaji wake huyo wa zamani.
Zahera amesema amefanya uchunguzi kutoka nchini Misri ambako Chirwa alikwenda kucheza soka na kubaini ameamua kuondoka huko baada ya klabu yake kushindwa kumlipa.
"Chirwa alikataa kucheza hapa kwa sababu alikuwa anadai mshahara. Aligoma kufanya mazoezi, akakataa kusafiri na timu akakosa mechi karibu tano," Zahera amesema katika mahojiano aliyofanya na Mwanaspoti
"Ameondoka, akaenda Misri baada ya miezi mitatu ameondoka huko pia kwa sababu hajalipwa mshahara kwa miezi mitatu. Anataka kurudi tena Yanga. Tuna uhakika gani kama hataondoka tena hapa kama hatalipwa?"
"Wale waliomtumia tiketi ya ndege mimi nawaangalia tu lakini Chirwa hatasaini mkataba kwenye timu yangu."
Zahera amesema kitendo cha Chirwa kurudi Yanga ni kama anarudi sehemu ambayo aliikimbia awali na kuleta usumbufu uleule.
Aidha Zahera amesema uwepo wa mshambuliaji huyo hapa nchini amejulishwa kwamba amevunja mkataba na klabu yake baada ya kushindwa kukubaliana katika malipo yake baada ya kuingia mkataba.
Licha ya kukataa kumsajili Chirwa, Zahera amesema Yanga itasajili mshambuliaji mwenye uwezo wa juu wakati wa dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa Novemba 15.

ADVERTISE HERE