Ratiba ya Yanga imeipa fursa timu hiyo kucheza michezo 11 mfululizo kwenye dimba la Taifa.
Yanga inatarajiwa kucheza mchezo wake wa kwanza nje ya Dar Disemba 03 mkoani Mbeya dhidi ya Prisons.
Baada ya Yanga kuendelea kupata matokeo mazuri kwenye michezo inayocheza uwanja wa Taifa, wapo wanaoamini hali hiyo inaweza kubadilika pale itakapoanza kucheza mikoani
Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema kwa wanaosubiri jambo hilo litokee wataendelea kusubiri sana kwani wamejiandaa na watahakikisha timu yao inafanya vizuri popote inapocheza.
"Watu wengi wanahofu juu ya kwamba tukienda kucheza mikoani tutapata wakati mgumu. Niseme kwamba matokeo yoyote unaweza kuyapata kulingana na ulivyojiandaa"
"Ukianza kusema kwamba Yanga itafanya vibaya mechi za ugenini, Yanga haijaanza leo kucheza ugenini. Miaka yote imekuwa ikicheza ugenini na inapata matokeo"
"Kutokupata matokeo ni sehemu ya mpira wa miguu lakini mwisho wa siku ni lazima ujiandae kupata matokeo," alisema Ten

ADVERTISE HERE