Yanga kamili kuikabili KMC leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Oct 2018
Yanga kamili kuikabili KMC leo
Leo Alhamisi mabingwa wa kihistoria wa Tanzania Yanga wanashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili KMC katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara mzunguuko wa 11.

KMC itakuwa mwenyeji wa mchezo huo unaotarajiwa kuanza saa moja usiku.

Yanga itakuwa inashuka dimbani kwa mara ya nane, ikiwa imeshinda michezo sita na kutoka sare mchezo mmoja mpaka sasa.

Ushindi utairudisha Yanga kwenye nafasi ya pili inayokaliwa na Simba ambayo jana iliwalaza vibonde Alliance kwa mabao 5-1

Kuelekea mchezo huo, jana kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera alisema wataikabili Mbao Fc kwa tahadhari kubwa.

KMC inanolewa na kocha Ettiene Ndayiragije ambaye kabla ya kutua katika timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu, alikuwa akiinoa Mbao FC.

Wakati akiinoa Mbao Fc, Ndayiragije anafahamika kwa kuwapa wakati mgumu Wana Jangwani kwani ndiye aliyeiwezesha Mbao kushinda michezo yote dhidi ya Yanga iliyopigwa kwenye dimba la CCM Kirumba.

Hata hivyo leo atakumbana na Yanga tofauti kabisa na ile aliyokumbana nayo miaka ya nyuma.

Zahera amesema malengo waliyojiwekea ni kuhakikisha wanapata matokeo mazuri kwenye michezo yote inayopigwa jijini Dar es salaam.

Kikosi cha Zahera kina majeruhi wawili tu Juma Mahadhi na Baruani Akilimali huku beki Andrew Vicent akitarajiwa kukosa mchezo huo kutokana na kufungiwa michezo mitatu
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
16h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
19h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
22h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’