Ligi Kuu ya Tanzania Bara mzunguuko wa 10 imeendelea leo kwa michezo mitatu kupigwa jijini Dar es salaam, Iringa na Mwanza.
Katika mchezo uliopigwa dimba la Taifa, Simba imeifunga Stand United mabao 3-0 wakati kule mkoani Iringa, Lipuli Fc imekubali kipigo cha bao 1-0 kwenye dimba lake kutoka kwa Kagera Sugar.
Mbao Fc nayo imeilaza Mtibwa Sugar bao 1-0 kwenye mchezo uliopigwa dimba la CCm Kirumba. Said Khamis akifunga bao kama la Ajib alilowafunga haohao Mbao Fc.

Baada ya kukamilika kwa michezo ya mzunguuko wa 10 (kwa baadhi ya timu), Azam Fc iko kileleni katika msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia alama 21.
Yanga imesalia nafasi ya pili ikiwa na alama 19 wakati Simba, Singida United, Mtibwa Sugar, JKT Tanzania na Mbao FC zinafuatia zote zikiwa na alama 17.
Azam Fc, Yanga, JKT Tanzania na Kagera Sugar ndio timu pekee ambazo mpaka sasa hazijapoteza mchezo kwenye ligi.

ADVERTISE HERE