Yanga yaongoza kwa kupachika mabao Ligi Kuu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Oct 2018
Yanga yaongoza kwa kupachika mabao Ligi Kuu
Licha ya kuwa imeshuka dimbani mara saba tu, Yanga inaongoza kwa kupachika mabao katika ligi kuu ya Tanzania Bara inayoendelea.

Ushindi wa mabao 3-0 iliyopata jana dhidi ya Alliance umeifanya timu hiyo ifikishe mabao 14.

Azam Fc inafuatia ikiwa imepachika mabao 12.

Jambo zuri zaidi katika kikosi cha Yanga ni kwamba timu hiyo imedhihirisha haitegemei mchezaji mmoja katika kupachika mabao.

Heritier Makambo na Ibrahim Ajib ndio vinara wakiwa wamefunga mabao matatu kila mmoja. Lakini Amisi Tambwe na Mrisho Ngasa nao wamefunga mabao mawili.

Kelvin Yondani, Andrew Vicent, Raphael Daudi na Deus Kaseke nao wamezifumania nyavu mara moja.

Ajib licha ya kuwa amefunga mabao matatu, pia ametengeneza mabao nane na hivyo kumfanya awe amehusika kwenye mabao 11 kati ya 14 yaliyofungwa.

Upande wa langoni, Beno Kakolanya ameruhusu bao moja katika michezo minne aliyocheza huku Klaus Kindoki akiruhusu mabao matatu yote akifungwa kwenye mchezo dhidi ya Stand United.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’