Yanga imeendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo nyumbani baada ya kuichapa Alliance Fc mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa Jumamosi jioni kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Ibrahim Ajib ameendelea kuwa mgodi wa mabao ya klabu ya Yanga baada ya leo kuhusika katika mabao yote matatu ya timu hiyo.
Bao la kwanza la Yanga lilifungwa na Heritier Makambo kwenye dakika ya 17 akiunganisha kwa kichwa krosi murua ya Ajib.

Ajib akamtengenezea Ngasa bao la pili kwenye dakika ya 24 ambapo mpira wake aliouvusha nyuma ya mabeki wa Alliance ulimaliziwa kwa urahisi na Ngasa aliyeuvusha juu ya mlinda lango aliyekuwa ametoka langoni.

Ajib akakamilisha kalamu ya mabao kwenye dakika ya 86 sasa akiukwamisha mpira kambani mwenyewe baada ya kupokea pasi murua kutoka kwa Deus Kaseke.
Yanga ilikuwa kwenye kiwango bora kabisa leo ikicheza kwa umakini mkubwa huku mlinda lango Beno Kakolanya akiokoa mipira kadhaa ya hatari langoni.
Kiungo Raphael Daudi na nahodha Kelvin Yondani walishindwa kumaliza mchezo huo baada ya kuumia na nafasi zao kuchukuliwa na Said Juma na Thabani Kamusoko.
Ngasa nae alitoka kwenye kipindi cha pili na nafasi yake kuchukuliwa na Deus Kaseke.
Ushindi huo umeipandisha Yanga hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 19 zikiwa ni alama mbili nyuma ya vinara Azam Fc.
Hata hivyo Yanga imeshuka dimbani mara saba tu.

ADVERTISE HERE