Kikosi cha Yanga leo Jumamosi kinashuka kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuikabili Allinace Fc katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara.
Yanga inayoshika nafasi ya tatu ikiwa na alama 16 baada ya kushuka dimbani mara sita, itakuwa inasaka ushindi wake wa sita msimu huu baada ya kuwa imeshinda michezo mitano na kutoka sare mchezo mmoja tu.
Aidha, ushindi utaiwezesha Yanga kufikisha alama 19 na kupanda nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi nyuma ya Azam Fc ambayo jana iliilaza African Lyon mabao 2-1 na kujikita kileleni baada ya kufikisha alama 21.
Hata hivyo Azam Fc imecheza michezo mitatu zaidi ya Yanga.
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera anatarajiwa kuwaongoza vijana wake kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuanza saa kumi kamili jioni.
Katika mchezo huo Yanga itawakosa Feisal Salum (kadi tatu za njano), Andrew Vicent (amefungiwa michezo mitatu) na Juma Mahadhi ambaye bado anauguza jeraha la goti baada ya kufanyiwa upasuaji kwa mara ya pili.

ADVERTISE HERE