Tshishimbi afunguka kilicho mchelewesha

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Aug 2017
Tshishimbi afunguka kilicho mchelewesha
Kiungo wa mpya wa Yanga, Papy Tshishimbi amewasili kisiwani Pemba tayari kuungana na kikosi hicho kinachojiandaa na mechi dhidi ya Simba itakayochezwa Jumatano ijayo kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Papy aliwasili Pemba saa 9:27 alasiri kwenye Uwanja wa Ndege wa Pemba na kupokelewa na meneja wa kikosi hicho Hafidh Saleh.

Akizungumza baada ya kuwasili Papy alisema ilikuwa afike mapema kujiunga na timu yake hiyo, lakini kikubwa kilichomzuia ni kuchelewa kwa pasi yake mpya ya kusafiria ambayo ilichelewa kutoka baada ya ile ya awali kuwa katika hatua za mwisho kumalizika.

Papy alisema pamoja na kuchelewa hajafanikiwa kuipata pasi hiyo kutokana na kulazimika kuwahi kujiunga na wenzake kujiandaa na mechi dhidi ya Simba.

Kiungo huyo anayetua Yanga akitokea Mbambane Swallows ya Swaziland alisema anahitaji kujifua kwa siku chache kuweka mwili.

Haikuwa kazi rahisi kwake kuondoka Mbambane kutokana na klabu hiyo bado inamuhitaji na kuwalazimu baadhi ya marafiki na mashabiki kulia na kuwapigia makelele viongozi wa klabu yake, lakini aliamua yeye binafsi kutaka kubadili maisha kwa kuhamia klabu nyingine.

"Nimefurahi sana kuwa hapa, nimekuja kuitumikia Yanga naamini nitafanya kazi ambayo mashabiki wa Yanga wataifurahia nimeambiwa walikuwa wananisubiri,"alisema Papy.

Kwa hisani ya Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
8h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
12h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
13h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
13h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
18h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’