Rais Magufuli aichangia Stars Mil 50

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Oct 2018
Rais Magufuli aichangia Stars Mil 50
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli amekabidhi fedha taslimu Mil 50 kwa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' ili zitumike katika maandalizi ya mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu fainali za michuano ya AFCON 2019 dhidi ya Lesotho utakaopigwa Novemba 16 huko Lesotho.

Rais Magufuli amekabidhi fedha hizo leo Ikulu jijini Dar es salaam katika hafla maalumu kufuatia mwaliko alioutoa kwa timu ya Taifa.

Rais Magufuli ameagiza fedha hizo zitumike kama chachu ya kuhakikisha Stars inaibuka na ushindi ugenini na inafanikiwa kufuzu kwa michuano ya AFCON 2019.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Rais Magufuli amesema yeye ni shabiki mkubwa wa timu ya Taifa lakini amekuwa hafurahiswi na matokeo mabaya inayopata timu hiyo.

"Watu wengi wamekataa tamaa kushabikia timu ya Taifa tupo zaidi ya 50M lakin tumeshindwa kupata watu 11 watakaotuletea kombe hapa Nyumbani," amesema Rais Magufuli

"Ndio maana wengi wanashabikia wachezaji wa nje, tunapongezana kwa mambo yasiyo na maana tunaitana Bungeni kujazana viburi tu.

"Viongozi wa soka wamekuwa wa hovyo inakatisha tamaa. Niliposikia uwanja wa ndege mdogo hauruhusu ndege yetu kutua Cape Verde nikasema vizuri kuliko kupeleka Ndege kule alafu tukafungwa! Nimewaita hapa pamoja na Viongozi wa michezo niwaambie ukweli.

"Nikafikiria kama timu zetu hazifanikiwi bora tuchukue wanajeshi tu wakawakilishe na niite timu ya Taifa maana timu zingine haziendi mbali.

"Lakini niseme ukweli naona timu yenu hii imeanza kuwa na matumaini hasa kipindi hiki cha Amunike ndio maana nimevutiwa nimeona niwaite," ameongeza Rais Magufuli

"Tulipofungwa tatu niliumia sana ndio maana hata Waziri sikumpongeza. Mkaja shinda mbili hapa wakati sisi tulifungwa tatu.

"Niliwashangaa hata mliokuwa mnashangilia, kwa sasa mmesema mnataka muanze mazoezi na wewe Nyoni(Alikuwa kiongoizi wa wachezaji) umesema mnaenda kushinda hivyoo nawaomba wachezaji hii iwe changamoto na pia Viongozi wa soka msimuingilie kocha yeye ndiye anajua nani acheze.

"Pia wachezaji waache uhuni na mambo mengine. Niwaombee Viongozi wa soka mfuatilie pesa tulizonyimwa na fifa , nami nitawaongezea Million 50.

"Natahadharisha, fedha hizo zitumike kwa ajili ya wachezaji na viongozi wale watakaoambatana na timu tu. Natata ushindi, mkishindwa mtazitapika kwa njia nyingine," aliweka msisitizo Rais Magufuli
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
17h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
21h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
22h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
22h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
2d ago
READ MORE β†’