Yanga 'kosi kama lote', ni mwendo wa bandika bandua

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
18 Oct 2018
Yanga 'kosi kama lote', ni mwendo wa bandika bandua
Achana na ufundi wa Feisal Salum ‘Fei Toto’ kiasi cha kumduwaza Kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike.

Unaambiwa huko Yanga kwa sasa mambo yamenoga na kilichobaki ni vijana wa Jangwani kufanya yao tu katika Ligi Kuu inayoendelea kesho.

Inaelezwa baada ya Gadiel Michael kujumuishwa kikosi cha Stars juzi dhidi ya Cape Verde, huenda akapumzishwa kwenye mchezo wa keshokutwa dhidi ya Alliance na Mwinyi Haji kuvaa uzi Jumamosi hii Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Lakini pia nyota wengine ambao hawakuwa wakipata nafasi katika kikosi cha kwanza wana nafasi kubwa ya kujumuishwa kwenye mchezo huo ambao Yanga watautumia kuendeleza rekodi yao ya kupototeza hata mchezo mmoja hadi sasa.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila aliwahakikishia nyota wake wa kikosi cha pili akiwamo Haji Mwinyi, Emmanuel Martin, Yusuf Mhilu kuvaa uzi Jumamosi dhidi ya Alliance na kuleta shangwe kwa vijana hao.

Mwandila amesema katika mchezo wao wa kirafiki wa kumuaga nahodha wao wa zamani Nadir Haroub ‘Cannavaro’ alitoa nafasi kwa nyota wake wanaoanzia benchi na kufanya vema kwa kuibuka na ushinfi wa 2-0 dhidi ya Malindi, huku akibaini mambo mazuri kutoka kwa wachezaji hao.

“Kuna baadhi ya wachezaji bado hawajaungana na timu baada ya kumaliza majukumu ya taifa, ila leo wanaweza kujiunga na wenzao katika mazoezi nafikiri watakuwa na siku mbili za mazoezi kabla ya kuwavaa Alliance naweza nikawapa mapumziko na kuwatumia nyota wengine niliokuwa nao pamoja tangu mwanzo wa maandalizi yetu,” Mwandila ameiambia tovuti ya Mwanaspoti

“Sipendi kumzungumzia mchezaji mmoja mmoja katika timu kikubwa ninachoweza kusema walifanya vizuri na ndio maana tuliweza kufanikiwa kuibuka na ushindi muda wao ukifika kucheza katika kikosi cha kwanza cha ligi watacheza kikubwa ni wachezaji wa Yanga na ndio maana muda wote wapo katika timu,” alisema.

PENGO LA DANTE

Beki wa kati wa Yanga, Andrew Vincent ‘Dante’ anatarajia kuwakosa Alliance katika mchezo unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi kutokana na kukabiliwa na adhabu aliyopewa na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la SOka nchini (TFF) kumfungia kucheza mechi tatu kutokana na utovu wa nidhamu kocha alisema ni pengo kubwa kwa timu lakini anaamini nyota waliopo watafanya vizuri.

“Ni mchezaji muhimu katika timu na amekuwa akitegemewa katika kikosi cha kwanza kukosekana kwake ni pengo lakini linaweza kuzimwa na wachezaji wanaocheza namba yake kwa kutumia nafasi ya kucheza vizuri na kumuaminisha mwalimu kuwa na wao wanaweza hata bila Dante,” alisema

“Yanga ina wachezaji wengi wazuri pamoja na kushindwa kupata nafasi ya kucheza wamekuwa wakijitahidi kupambana mazoezini lengo ni kuhakikisha wanatushawishi waalimu tuweze kuwapa nafasi sasa ni wakati wao sahihi kuonyesha watanzania pamoja na mashabiki wa timu kuwa sio Dante tu ambaye amezaliwa kwaajili ya kuisaidia Yanga katika nafasi hiyo,” alisema.

AJIBU ASHANGAZA

Tofauti na alivyozoeleka Ibrahim Ajibu kuonekana ni mtu mwenye kutega mazoezi na alishaingizwa katika listi ya nyota kadhaa wanaokatwa mishahara kutokana na kukosa mazoezi, hali imekuwa tofauti sasa kiasi cha kumshangaza kocha Mwandila.

Mwandila alisema Ajibu amekuwa mchezaji wa kwanza kufika mazoezi na amekuwa akiwahimiza wenzake, jambo ambalo ni mabadiliko makubwa kwa mchezaji huyo na kumtabiria makubwa hapo mbele kama ataendelea kufanya hivyo.

“Huwezi kuamini Ajibu tangu tumeanza Jumatatu siku moja baada ya kutoka Zanzibar tayari kujiandaa na mchezo dhidi ya Alliance, ndiye anayeongoza kwa kuwahi mazoezi na muda mwingine anaonekana kuwahimiza wenzake ni tofauti na nilivyomzoea ni mtu ambaye alikuwa anapenda kutega na kutoa sababu zisizokuwa na msingi.”

FEI TOTO NOMA

Katika hatua nyingine mpira mwingi alioupiga kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ ndani ya dakika 32 alizopewa na Kocha Amunike wa Taifa Stars zimemkuna kocha huyo na kumwagia sifa.

Feisal anayekipiga Yanga, aliingia akichukua nafasi ya Mudathir Yahya dakika 58 katika mechi dhidi ya Cape Verde na kubadilisha kabisa mchezo kutokana na jinsi alivyocheza kwa kutoa pasi za uhakika na kulainisha safu ya kiungo pale katikati.

Kocha Amunike alisema jinsi Fei alivyoitwa Stars mazoezini alikuwa anafanya vitu vya kawaida, ila alimwambia Stars ni kama Ligi ya Italia anatakiwa apambane na ameonyesha.

“Alinisikia na kunielewa na hata alipoingia alifanya timu ikae sawa katika upande wa kiungo na hiki ndicho ambacho tunakihitaji katika timu yetu.” Alisema.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
3h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
8h ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
12h ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
13h ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
13h ago
READ MORE →
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
13h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE →
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE →
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE →
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE →