Klabu ya Yanga ikiongozwa na Kaimu Mwenyekiti Clement Sanga na Katibu Mkuu Charles Mkwasa imekutana na Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kujadili mustakabali wa deni la zaidi ya Mil 300 inayodaiwa Yanga na Wizara hiyo ikiwa ni malimbikizo ya kodi ya kiwanja kinachomilikiwa na klabu hiyo.
Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema klabu imefikia Makubaliano na Wizara ya Ardhi juu ya utaratibu wa kulipa deni hilo.
Amesema Yanga imeridhia kulipa deni hilo katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja, Serikali imekubaliana na mpango huo ambapo pande zote zimesaini mkataba wa makubaliano.

ADVERTISE HERE