Yanga na Simba 'zagongana' kwa Kahata

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Oct 2018
Yanga na Simba 'zagongana' kwa Kahata
Wakati dirisha dogo la usajili linakaribia kufunguliwa, uongozi wa Yanga umeingia kwenye mpambano na watani zao Simba katika kuwania saini ya kiungo wa Gor Mahia na timu ya Taifa ya Kenya (Harambee Stars), Francis Kahata.

Inaelezwa kiungo huyo alikuwa tayari amekamilisha mazungumzo na Simba na ilielezwa kuwa atajiunga na mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara itakapofika Desemba mwaka huu baada ya awali klabu yake kuhitaji kiasi kikubwa cha fedha ili kuvunja mkataba.

Taarifa zilizopatikana jijini Dar es Salaam zinaeleza kuwa, Yanga pia imefikia hatua nzuri za mazungumzo na mchezaji huyo na kama Simba "itazubaa" nyota huyo ataonekana Jangwani.

"Yanga tunafanya mambo yetu kimya kimya, si wanajua hatuna fedha, lakini makamanda wetu wanaendelea na kazi, tunaelekea vizuri na usajili wa Kahata pamoja na yule beki wa Rayon (Abdul Rwatubyaye)," kimesema chanzo.

Naye Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Said Tully, ameliambia gazeti la Nipashe kuwa klabu yao bado haijavunja mawasiliano na Kahata na wanaamini atatua Msimbazi na kuwasaidia kupeperusha bendera ya Bara kwenye mashindano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

"Sio rahisi akaenda Yanga, bado yuko katika mazungumzo na sisi, na vile vile ana mipango mingine ya kwenda Ulaya, ana ofa ziko mikononi," alisema Tully.

Klabu hizo zimekuwa na tabia ya kuvurugiana mipango ya usajili na endapo timu mojawapo itazidiwa nguvu ya fedha au itazubaa inakuwa imepoteza nafasi ya kumsajili mchezaji huyo.

Kahata alizivutia timu hizo baada ya kuonyesha uwezo wa juu katika mashindano ya SportPesa na Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) na vile vile kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga tayari ilishaanza mazungumzo ya kumsajili Mnyarwanda Rwatubyaye, lakini taarifa kutoka Rwanda zinaeleza kuwa beki huyo wa Amavubi pia ameanza mchakato wa kwenda kucheza soka la kulipwa huko Ubelgiji.

Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Yanga na Simba kuingia katika vita ya kuwania wachezaji.

Usajili uliopita Yanga ilimsajili kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' baada ya kumnyakua kutoka mikononi mwa viongozi wa Simba.

Pia wachezaji wengi waliosajiliwa na Simba msimu huu walikuwa wakiwaniwa na Yanga.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
7h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’