Kiungo wa Yanga Feisal Salum 'Fei Toto' jana alipata nafasi ya kuitumikia timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kwenye mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu fainali za AFCON 2019.
Fei Toto aliingia kwenya dakika ya 68 kuchukua nafasi ya Mudathir Yahya Abbasi katika mchezo ambao Stars iliibuka na ushindi wa mabao 2-0
Kilichowafurahisha wengi ni uwezo mkubwa wa kumiliki mpira ulioonyeshwa na kinda huyo mwenye umri wa miaka 20.
Fei Toto alionyesha uhodari wake katika kuchezea mpira, upigaji wa pasi na uwezo mkubwa wa kufanya maamuzi anapokuwa na mpira.
Fei Toto amedhihirisha ni mmoja wa wachezaji ambao watakuwa tegemeo kwa timu ya Taifa siku za usoni.
Kocha wa Stars Emmanuel Amunike amesifu kiwango kilichoonyeshwa na kiungo huyo.

ADVERTISE HERE