Wakati zikiwa zimebaki takribani wiki nne kabla ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa, zimeripotiwa taarifa kuwa baada ya mapendekezo kutolewa na Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera, uongozi wa timu hiyo umekusudia kuchukua 'maamuzi magumu' dirisha la usajili litakapofunguliwa.
Kulingana na taarifa hizo, uongozi una mpango wa kuachana na wachezaji ambao viwango vyao vimeshuka/haviridhishi na hawana tena msaada kwa timu.
Kwamba Yanga imekuwa ikitumia gharama kubwa kuwalipa mishahara wachezaji hao ambao kwa sasa hawana hadhi ya kuendelea kubaki Jangwani.
Panga hilo pia linakusudia kuwaondoa wachezaji hao ili kusajili wachezaji wengine wenye uwezo mkubwa kuchukua nafasi zao.
Je kwa mtazamo wako unadhani kuna wachezaji wanastahili kuondolewa Jangwani kwa kuwa wanakula mshahara wa bure?
Kwa mtazamo wangu naona kikosi cha Yanga kiko sawa sawa sana wakati huu. Kinahitaji maboresho machache sana hasa upande wa beki na safu ya ushambuliaji.
Baadhi ya wachezaji wanaweza kuonekana hawana msaada kwa kuwa hawapati nafasi ya kucheza. ushindani wa namba umekuwa mkali sana.
Lakini upande wa safu ya ulinzi nadhani kuna ulazima wa kuiongezea nguvu zaidi.
Yanga inawategemea mabeki wawili zaidi, Chikupe na Yondani ambapo wakikosekana ni majanga.
Abdallah Shaibu ameendelea kupata uzoefu lakini bado anahitaji muda zaidi ili aweze kuaminiwa kama ilivyo kwa wakubwa zake hao.
Kwenye safu ya ushambuliaji, Heritier Makambo na Tambwe ndio washambuliaji wanaotegemewa zaidi.
Wengi wamekuwa na matumaini makubwa kwa Makambo lakini nae ameonekana atahitaji muda zaidi. Alianza vizuri, lakini kasi yake imepungua. Amekuwa akikamiwa na mabeki baada ya kusifiwa sana.
Tambwe hatabiriki, majeraha yamemfanya asiaminiwe tena ingawa hakuna shaka bado anao uwezo wa kupasia mipira nyavuni.
Alilidhihirisha hilo kwenye mchezo dhidi ya Singida United alipofunga mabao yote mawili ya Yanga.
Nawe Mwana Jangwani unadhani ni mabadiliko gani Yanga inaweza kukifanyia kikosi chake ili kiweze kuimarika zaidi?

ADVERTISE HERE