Chikupe, Kotei wafungiwa mechi tatu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Oct 2018
Chikupe, Kotei wafungiwa mechi tatu
Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limetoa adhabu ya kutocheza mechi tatu na faini ya Sh 1 milioni kwa kiungo wa Simba, James Kotei na beki wa Yanga, Andrew Vincent 'Dante' kutokana na utovu wa nidhamu.

Wawili hao walifikishwa mbele ya kamati hiyo kutokana na makosa hayo waliyoyafanya katika mchezo wa Watani wa Jadi Simba na Yanga uliofanyika Septemba 30, uliomalizika kwa suluhu.

Kotei alishtakiwa kwa kosa la kumpiga ngumi, beki Gadiel Michael wakati walipokuwa wakiwania mpira wakati Dante alituhumiwa kumpiga kichwa nahodha wa Simba, Mohammed Hussein 'Tshabalala' matukio ambayo hayakutolewa adhabu na mwamuzi wa mchezo huo, Jonesia Rukyaa kutoka Kagera.

Kwa mujibu wa tovuti ya Mwanaspoti, uamuzi wa kuwafungia wachezaji hao sambamba na kuwatoza faini hiyo umechukuliwa na kikao cha kamati ya nidhamu ya TFF kilichoketi hivi karibuni ambacho kilibaini kuwa nyota hao wawili wamevunja kanuni ya udhibiti wa wachezaji ya Ligi Kuu toleo la 2018.

Kanuni hiyo inafafanua kuwa mchezaji yeyote atakayekutwa na hatia ya kupiga au kupigana, atafungiwa idadi hiyo ya mechi pamoja na kiwango hicho cha faini.

Hata hivyo, kwa mujibu wa faini waliyotozwa wachezaji hao ni kubwa kulinganisha na ile iliyoainishwa na kanuni hiyo.

Mchezaji atakayetolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kosa la kupiga/kupigana atasimama kushiriki michezo mitatu (3) ya klabu yake na atalipa faini ya Sh 500,000," kinafafanua kifungu cha tatu cha kanuni namba 38 ya udhibiti wa wachezaji.

Akizungumzia kuhusu adhabu hiyo, Kotei alisema uamuzi wa mwisho utatolewa na klabu yake.

"Nimesikia kuhusu hiyo adhabu, lakini siwezi kuizungumzia chochote na badala yake kama nitakata rufaa au la ni klabu ndiyo itaamua," alisema Kotei.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’