Fei Toto ataikosa Alliance, Chikupe hatihati

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Oct 2018
Fei Toto ataikosa Alliance, Chikupe hatihati
Wakati kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' atakosa mchezo dhidi ya Alliance Jumamosi ijayo kutokana kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano, Yanga pia inaweza kumkosa beki wake kisiki Andrew Vicent Chikupe aliyepelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF akituhumiwa kumpiga kichwa Mohammed Hussein kwenye mchezo wa watani wa jadi.

Mratibu wa Yanga Hafidh Saleh amesema timu hiyo inafahamu haitakuwa na Fei Toto kwenye mchezo ujao wa ligi dhidi ya Alliance kufuatia kuonyeshwa kadi za njano katika michezo dhidi ya Stand United, Singida United na Mbao FC.

Lakini pia bado hawajafahamu hatma ya Chikupe ambaye alipelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF sambamba na mchezaji wa Simba James Kotei wakituhumiwa kufanya matukio ya utovu wa nidhamu kwenye mchezo wa watani wa jadi.

Hata hivyo kiungo Papi Kabamba Tshishimbi aliyekosa mchezo dhidi ya Mbao Fc kutokana na majeruhi amerejea kikosini.

Lakini kwa jinsi Yanga ilivyoimarika, kukosekana kwa Fei Toto hakuwezi kuwa tatizo kwa kikosi cha Mwinyi Zahera ambacho kina wachezaji wengine wanaoweza kucheza nafasi yake.

Pato Ngonyani na Said Juma Makapu walin'gara kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Malindi uliopigwa visiwani Zanzibar juzi, wanaweza kuwa mbadala wa Fei Toto.

Ukimuondoa Tshishimbi ambaye anaweza kucheza popote kwenye safu ya kiungo, wapo viungo wengine kama Thabani Kamusoko, Raphael Daudi na Maka Edward mbao wanaweza kutumika pia.

Yanga inajifua kwenye uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam chini ya kocha wake msaidizi Noel Mwandila.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’