Zahera kuiwahi Alliance Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Oct 2018
Zahera kuiwahi Alliance Fc
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera atauwahi mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara kati ya Yanga dhidi ya Alliance utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa Jumamosi ijayo, Oktoba 20.

Zahera kwa sasa yuko nchini Zimbabwe na kikosi cha timu ya Taifa ya DR Congo ambayo kesho Jumanne itashuka dimbani kusaka tiketi ya kutinga fainali za AFCON 2019.

DR Congo inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi G ikiwa na alama nne nyuma ya vinara Zimbabwe wenye alama saba.

Juzi Jumamosi DR Congo ilikubali kipigo cha mabao 2-1 nyumbani kutoka kwa Zimbabwe.

Zahera anatarajiwa kurejea Jumatano kuendelea kukiandaa kikosi cha Yanga kinachoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya kushinda michezo mitano na kutoka sare mchezo mmoja.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’