Ni kawaida sana kwa mchezaji anapotoka timu moja kwenda nyingine kuanza taratibu na wengine huchukua muda mrefu zaidi kuzoea mazingira ya timu mpya.
Mchezaji anapohamia kwenye timu mpya anakutana na mazingira tofauti kabisa na kule alikotoka. Hii ni kuanzia wachezaji wenzake, mifumo na hata aina ya mazoezi wanayopewa.
Mwanzoni wapo waliomuangalia Ibrahim Ajib kwenye ule mchezo wa kwanza wa kirafiki dhidi ya Singida United na kumbeza kuwa hatakuwa na msaada wowote kwa Yanga.
Licha ya ukweli kwamba Ajib amekuwa akifanya vizuri sana kwenye mazoezi ya kikosi cha Yanga, amekuwa akifunga mabao mara kwa mara.

Lakini sasa taratibu ameanza kuwanyamazisha wale waliokuwa wanambeza kwani ameendelea kuwa msaada mkubwa kwa Yanga kwa kuifungua mabao.
Katika michezo miwili ya kirafiki iliyopita, Ajib amefunga kwenye kila mchezo na anaonekana kwenda sambamba na mifumo ya kocha wa Yanga, George Lwandamina.
Ajib ana kipaji cha hali ya juu hakika msimu huu anaweza akawa mmoja wa wafungaji vinara kwenye ligi.
Uwepo Ibrahim Ajib, Amissi Tambwe, Donald Ngoma na Obrey Chirwa kwenye kikosi cha Yanga ni habari mbaya kwa timu zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom msimu huu.

ADVERTISE HERE