Yanga imefanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Malindi FC katika mchezo wa kirafiki uliopigwa leo Jumamosi jioni kwenye dimba la Amaan visiwani Zanzibar.
Mchezo huo uliokuwa maalum kwa ajili ya kumuaga nahodha wa zamani wa Yanga Nadir Haroub 'Cannavaro', ulitanguliwa na tukio la kumpa heshima mkongwe huyo aliyestaafu soka na kisha kukabidhiwa majukumu ya Umeneja wa Yanga.

Yanga ilijipatia mabao yake kwenye kila kipindi ambapo bao la kwanza lilifungwa na Emmanuel Martin kwenye dakika ya 43 akimalizia pasi ya Mrisho Ngasa aliyekuwa mwiba kwa safu ya ulinzi ya Malindi.
Ngasa aliifungia Yanga bao la pili kwenye dakika ya 60 akimalizia krosi iliyopigwa na Pius Buswita kutoka upande wa kulia.
Yanga ilitumia mchezo huo kuwapa nafasi wachezaji wake wote ambao wamekuwa hawapangwi kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Aidha, Yanga ilifanya mabadiliko kwa nyakati tofauti kuwapa nafasi wachezaji wote waliosafiri na kikosi cha timu hiyo visiwani Zanzibar

ADVERTISE HERE