FT : Cape Verde 3-0 Tanzania

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Oct 2018
FT : Cape Verde 3-0 Tanzania
Mabao mawili yaliyofungwa na Ricardo Gomez na moja la Tavares yameihakikishia Cape Verde ushindi muhimu wa mabao 3-0 nyumbani dhidi ya Tanzania.

Mchezo huo wa kusaka tiketi ya kutinga fainali za michuano ya AFCON 2019 umeishuhudia Stars ikipoteza mchezo wake wa kwanza kundi L.

Kipindi cha kwanza hakikuwa kizuri sana kwa vijana wa Emmanuel Amunike lakini waliimarika katika kipindi cha pili na kupeleka mashambulizi mengi langoni kwa Cape Verde.

Hata hivyo Cape Verde walimiliki mpira kwa muda mwingi na kutengeneza nafasi nyingi zaidi.

Ni ushindi ambao wameustahili kutokana na juhudi kubwa walizoonyesha katika ardhi yao ya nyumbani.

Walikuwa timu bora kwenye mchezo huo.

Ushindi huo umeipelekea Cape Verde kileleni mwa kundi L baada ya kufikisha alama nne sawa na Uganda lakini Cape Verde imejiongezea mtaji wa mabao baada ya ushindi wa leo.

Uganda itakuwa nyumbani kesho kuchuana na Lesotho.

Stars sasa itahitaji kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa Jumanne ijayo katika dimba la Taifa ili kuweka hai matumaini ya kufuzu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
2h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
17h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
20h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’