Tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara maarufu nchini Mohammed Dewji 'MO' ambaye ni mwekezaji wa klabu ya Simba limeitikisa Tanzania.
Aidha tukio hilo lililotokea Alfajiri ya leo Alhamisi, Oktoba 11 2018 limeripotiwa na karibu vyombo vyote vya habari vya Kimataifa zikiwemo televisheni za CNN, BBC na Aljazeera.
Ni tukio la kusikitisha ambalo linaweza kuitia doa Tanzania kwenye medani ya Kimataifa kwani linaweza 'kuwaogofya' wawekezaji waliokuwa na dhamira ya kuja kuwekeza nchini wakihofia usalama.
Jeshi la Polisi linaendelea kuwasaka wahalifu waliohusika katika tukio hilo ambapo Kamanda wa Polisi kanda Maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa amesema tayari kuna watuhumiwa wametiwa nguvuni.
Tunalaani vikali tukio hili lisilo la kiungwana. Tuna imani na jeshi letu la polisi pamoja na vyombo vyote vya ulinzi na usalama watampata MO akiwa salama.
Aidha, tunaungana na familia ya MO na wenzetu wa Simba. Tunawapa pole na tuko pamoja nao katika kipindi hiki kigumu.

ADVERTISE HERE