Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuelekea visiwani Zanzibar kuendelea na maandalizi ya michezo ya ligi kuu ya Tanzania Bara.
Keshokutwa Jumamosi, Oktoba 13, 2018 inatarajiwa kucheza na Malindi Fc katika mchezo maalum wa kumuaga mkongwe Nadir Haroub 'Cannavaro' ambaye sasa ni Meneja wa timu hiyo.
Mratibu wa Yanga Hafidh Saleh amesema walipokea mwaliko kutoka klabu ya Malindi kucheza mchezo wa kirafiki visiwani humo ambao pia utatumika kumuaga Nadir.
Aidha ikiwa Zanzibar Yanga itamtembelea Mama Fatma Karume, mmoja wa wadhamini wa klabu hiyo.
Yanga inayoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi itarejea jijini Dar es salaam mwanzoni mwa wiki ijayo tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Alliance utakaopigwa uwanja wa Taifa, Oktoba 20

ADVERTISE HERE