Emmanuel Martin apania kumshawishi Zahera ampe nafasi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Oct 2018
Emmanuel Martin apania kumshawishi Zahera ampe nafasi
Wakati Yanga ikinolewa na Kocha George Lwandamina, winga Emmanuel Martin alikuwa amejihakikishia namba kwenye kikosi cha kwanza cha Mzambia huyo.

Hata kwenye michezo ya mwanzoni ya kocha Mwinyi Zahera, Martin alikuwa akipata nafasi hasa kwenye michuano ya kombe la Shirikisho.

Lakini sasa mambo yamebadilika kwani winga huyo ni nadra sana kumuona hata kwenye orodha ya wachezaji wa akiba kutokana na ushindani mkali wa namba kwenye kikosi cha Zahera.

Mwenyewe hali hiyo haifurahii na amekuwa akiitumia kama changamoto ya kujituma zaidi ili aweze kumshawishi Zahera amrudishe kwenye kikosi cha kwanza.

"Si kitu kizuri kwa mchezaji kutocheza, inaniumiza na kunifunza kujituma kwa bidii ili niweze kumshawishi kocha ili kunipa nafasi ya kucheza.

"Msimu huu kwangu unanifanya niwaze mbali zaidi, tofauti na uliopita ambao nilikuwa na nafasi kubwa, naendelea kujituma ili msimu huu usinipite bure, hii ndio kazi ninayoitegemea" Martin amenukuliwa na gazeti la Mwanaspoti

Msimu huu Yanga imeongeza wachezaji saba kwenye kikosi chake.

Klaus Kindoki, Deus Kaseke, Mrisho Ngasa, Heritier Makambo na Feisal Salum wameingia moja kwa moja kwenye mipango ya Mwalimu huku Jaffar Mohammed naye akiwa bado hajapata nafasi kwenye kikosi cha Mcongo huyo.

Mohammed Issa 'Banka' bado hajaanza kuitumikia Yanga licha ya kusajiliwa kukiwa na tetesi kuwa mchezaji huyo amefungiwa.

Ujio wa wachezaji wapya umepelekea kwa baadhi ya wachezaji waliokuwa wanapata nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza kuwa na wakati mgumu.

Miongoni mwa wachezaji hao ni pamoja na Ramadhani Kabwili, Maka Edward, Said Juma, Said Mussa, Baruani Akilimali, Haji Mwinyi, Emmanuel Martin, Yohana Mkomola na Pius Buswita.

Katika moja ya mahojiano yake Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera alisema hakusudii kuacha mchezaji wakati wa dirisha dogo la usajili lakini huenda akaridhia kuwatoa kwa mkopo baadhi ya wachezaji ili kulinda viwango vyao.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’