Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wakili Revocatus Kuuli amejiuzulu kuongoza kamati.
Uuongozi wa shirikisho hilo umesema kujiuzulu kwake siyo tatizo kwao kazi zitaendelea kama kawaida.
Kuuli amejiuzulu nafasi hiyo ikiwa ni siku chake tu tangu Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidau amwandikie barua ya kujieleza ndani ya siku tatu akieleza kwa nini amesimamisha uchaguzi wa Simba.
Hata hivyo katika taarifa ya Kuuli alisema tarehe ya uchaguzi ya Simba itabaki ile ile iliyopangwa na Kamati ya Uchaguzi ya Simba ila wafanye marekebisho baadhi ya kanuni ambazo zipo kinyume na kanuni za uchaguzi za TFF.
Kuuli amesema hawezi kuendelea kuongoza Kamati hiyo kwa kile alichodai ni kuwepo na ubabaishaji na kuingiliwa na majukumu ya Kamati wakati yeye anasimamia sheria.
Makamu wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani alizungumzia kujiuzulu kwa Kuuli kwamba hakutapunguza wala kuongeza jambo lolote ndani ya TFF.
"Amejiuzulu Kuuli na siyo kamati nzima, kuna makamu wake ambaye ataendelea na majukumu hayo ya kusimamia chaguzi zilizopo na kazi zingine za Kamati, hivyo hakuna tatizo lolote na kila kitu kinakwenda kama kilivyopangwa," alisema Nyamlani.

ADVERTISE HERE