Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kinatarajiwa kuondoka leo saa tano usiku kwenda Cape Verde kwa ajili ya mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu kwa fainali za AFCON 2019 dhidi ya wenyeji wao Cape Verde.
Mchezo huo utapigwa Ijumaa ya wiki hii, Oktoba 12, 2018.
Stars inakwenda Cape Verde kwa usafiri wa ndege maalum iliyotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ndege hiyo itairejesha Stars nchini baada ya mchezo huo tayari kwa mchezo wa marudiano dhidi ya Cape Verde utakaopigwa uwanja wa Taifa Jumanne ijayo, Oktoba 16 2018.

ADVERTISE HERE