Beki wa kushoto wa Yanga Gadiel Michael amesema Ibrahim Ajib, kiungo fundi wa timu hiyo ndio mchezaji anayemkubali zaidi hapa Tanzania.
Gadiel amesema Ajib ni mchezaji asiyetabirika, anaweza kufanya jambo la kuinufaisha timu wakati wowote anapokuwa dimbani.
"Namkubali sana Ajib kwa hapa Tanzania," amesema.
"Ukiwa nae dimbani anaweza kuipa timu matokeo wakati wowote."
Kauli ya Gadiel imekuja siku moja baada ya Ajib kuisaidia Yanga kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbao FC.
Ajib alitengeneza bao la kwanza kisha mwenyewe kufunga bao la pili kwa uhodari wa hali ya juu.
Bao hilo tayari limeingizwa kwenye rekodi ya mabao bora yaliyofungwa kwenye ligi kuu ya Tanzania Bara.
Haitakuwa jambo la kushangaza kama bao hilo litaibuka kuwa bao bora la msimu mwishoni mwa msimu kutokana na unadra wake.
Mabao kama alilofunga jana Ajib hufungwa mara chache sana duniani. Pengine mara moja katika msimu mzima.

ADVERTISE HERE