Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema ameshitushwa na tangazo lililotolewa na Kampuni ya Msolopa iliyopewa idhini ya kupiga Mnada Jengo la Yanga kutokana na deni la zaidi ya Mil 300.
Mkwasa amesema Yanga ilifanya makubaliano na Wizara ya Ardhi juu ya utaratibu wa kulipa deni hilo kwa kutumia mapato inayopata mlangoni katika mechi zake.
"Ni kweli tuna deni kubwa tunadaiwa la ardhi, lakini tayari tulifanya nao mazungumzo na kukubaliana namna ya kulilipa kupitia mapato yetu ya milangoni.
"Lakini tatizo ni kwamba hapa katikati Ligi ilisimama, lakini hivi karibuni inaanza na tutaendelea kulipa,"amesema.
Yanga inalipa kodi ya ardhi wastani wa Mil 56 kwa mwaka. Mkwasa amekiri kodi hiyo haijalipwa kwa miaka kadhaa.

ADVERTISE HERE