Naamini kocha ataniita timu ya Taifa awamu ijayo - Ajib

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Oct 2018
Naamini kocha ataniita timu ya Taifa awamu ijayo - Ajib
Kiungo mshambuliaji wa Yanga Ibrahim Ajib ndio 'habari ya mjini' kwa sasa baada ya hapo jana kufunga moja ya mabao ya msimu.

Licha ya kufunga, Ajib alihusika katika utengenezaji wa bao la kwanza la Yanga kwenye ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbao FC.

Tangu kuanza kwa msimu huu Ajib amekuwa akiifanya kazi ya kutengeneza na kufunga mabao kwanye kikosi cha Yanga kwa umahiri mkubwa. Akiwa ametengeneza mabao sita na kufunga mawili.

Hata hivyo kiungo huyo hakuitwa na kocha Emmanuel Amunike kwenye kikosi cha timu ya Taifa 'Taifa Stars' kinachojiandaa na michezo miwili ya kusaka tiketi ya kufuzu kwa michuano ya AFCON 2019 dhidi ya Cape Verde.

Akizungumza baada ya mchezo wa jana, Ajib amesema kutoitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa kwake ni changamoto inayomfanya aongeze juhudi zaidi.

"Kutoitwa timu ya Taifa kwangu ni changamoto. Inanifanya niongeze bidii zaidi ili niweze kufanya vizuri na naamini wakati ujao kocha ataniona"
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
23h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’