Taarifa za 'chinichini' zinabainisha kuwa kuna jitihada zinafanywa na uongozi wa Yanga kumuongeza aliyekuwa kocha msaidizi wa Simba Masudi Djuma katika benchi la ufundi.
Inaelezwa Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amevutiwa na uwezo wa kocha huyo na amependekeza aongezwe kwenye benchi la ufundi la timu hiyo.
Yanga bado haina kocha Msaidizi (Wa Kuajiriwa) tangu ilipoachana na Shedrack Nsajigwa aliyetimkia Singida United.
Noel Mwandila anayekaimu nafasi hiyo sasa aliajiriwa kama kocha wa viungo.
Djuma amefikia makubaliano ya kuvunja mkataba wake na uongozi wa klabu ya Simba jana baada ya kudaiwa kutokuwa na maelewano mazuri na kocha mpya wa timu hiyo Patrick Aussems.

ADVERTISE HERE