Yanga 'inakimbiza' Afrika Mashariki kwa rekodi za kushiriki michuano ya CAF

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Oct 2018
Yanga 'inakimbiza' Afrika Mashariki kwa rekodi za kushiriki michuano ya CAF
Yanga haitashiriki michuano yoyote ya kimataifa kwa msimu ujao inayotarajiwa kuanza mwezi wa 11 baada ya kushindwa kufuzu msimu uliopita.

Lakini asikuambie mtu mabingwa hao wa Kihistoria wameipiga bao watani zao, Simba nje ndani.

Yanga imewekea rekodi mbili ngumu ambazo watani wake Simba na timu nyingine nane kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki zitapaswa kufanya kazi ya ziada kuzivunja.

Klabu 10 za Afrika Mashariki licha ya kufanikiwa kukata tiketi ya kushiriki kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho msimu ujao, kirekodi zimeonekana kushindwa kufua dafu mbele ya Yanga ambayo haitoshiriki baada ya kufanya vibaya kwenye Ligi Kuu na Kombe la FA msimu uliopita.

Rekodi ya kwanza ya Yanga ambayo klabu hizo za nchi za Burundi, Rwanda, Kenya, Uganda na Tanzania ikiwemo Simba, zinapaswa kuivunja ni ya kufuzu mara nyingi zaidi katika hatua ya makundi ama ya Ligi ya Mabingwa Afrika au Kombe la Shirikisho.

Ukiondoa KCCA ya Uganda ambayo inaonekana ndio timu pekee Afrika Mashariki inayoweza kupindua rekodi ya Yanga ikiwa nayo imefuzu mara mbili hatua ya makundi Kombe la Shirikisho au Ligi ya Mabingwa, kuanzia mwaka 2000 hadi sasa hakuna nyingine yoyote ya Ukanda huu iliyofanya hivyo.

Wakati Yanga ilifuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho 2016 kabla ya kufanya hivyo tena mwaka huu, KCCA yenyewe ilifuzu makundi ya Shirikisho Afrika 2017 kabla ya mwaka huu kufuzu hatua hiyo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Rekodi nyingine ambayo Yanga inatamba nayo ni ya kushiriki kwenye mashindano ya klabu Barani Afrika mara nyingi zaidi kuliko timu nyingine katika kipindi cha miaka 18, kinachoanzia mwaka 2000 hadi sasa.

Katika kipindi hicho, Yanga imeshiriki mara 15, Simba yenyewe imeshiriki mara 12 na hivyo ushiriki wake msimu ujao, utaifanya idaiwe na Yanga kushiriki mara moja nyingine ili waende sawa.

Ukiondoa Simba na KCCA, timu nyingine zitakazowakilisha ukanda huo wa Afrika Mashariki ni Le Messager Ngozi na Vital'O (Burundi), Vipers (Uganda), APR na Mukura (Rwanda), Mtibwa (Tanzania) na Gor Mahia (Kenya)

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
20h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’