Yanga yaitaka TFF imchukulie hatua Kotei

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Oct 2018
Yanga yaitaka TFF imchukulie hatua Kotei
Uongozi wa klabu ya Yanga umelitaka Shirikisho la soka nchini (TFF) kumchukulia hatua kiungo wa Simba James Kotei kufuatia tukio lake la kumpiga ngumi mlinzi wa kushoto wa Yanga Gadiel Michael kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara kati ya watani wa jadi, uliopigwa uwanja wa Taifa Jumapili iliyopita.

AKizungumza na waandishi wa habari leo Makao Makuu ya Yanga yaliyoko Mtaa wa Twiga na Jangwani jijini Dar es salaam, Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema wameiandikia barua TFF wakieleza kusikitishwa na tukio hilo.

Ten amesema tukio hilo halikuwa la kiungwana na wasingependa kuona matukio ya aina hiyo yanaendelea kutokea hivyo wameitaka TFF imchukulie hatua Kotei kwa mujibu wa kanuni na taratibu zilizopo.

"Kama klabu hatuwezi kukaa kimya kwa vitendo ka hivyo vinatokea, tumeandika barua..

"Sasa tutawaachia TFF wenyewe tuone kama wanachukua hatua au la, lakini sisi tumeonyesha namna tulivyokerwa na vitendo ambavyo si vya kiungwana," alisema.

TFF kupitia Kamati yake ya saa 72 bado haijatoa taarifa kuhusu tukio hilo ambalo licha ya kutoonwa na mwamuzi, kamera za Azam TV ziliweza kumnasa Kotei akimpiga ngumi ya mgongo Gadiel Michael.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’