Hili la wachezaji kutoka kambini Stars kwenda kuzitumikia timu zao mmh..

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Oct 2018
Hili la wachezaji kutoka kambini Stars kwenda kuzitumikia timu zao mmh..
Duniani kote wachezaji wa vilabu wanapoitwa timu za Taifa na kuingia kambini ni nadra sana kusikia wachezaji hao wanaruhusiwa kwenda kuzitumikia timu zao kisha kurejea tena kambini.

Pengine huu ni utaratibu mpya ambao Shirikisho la soka nchini TFF limeamua kuanzisha lakini sidhani kama upo mahali pengine popote.

Kama kuna ulazima wa kambi ya timu ya Taifa kuanza mapema kwa nini TFF isifute michezo ya baadhi ya timu ambazo zina wachezaji wengi kwenye timu ya Taifa kama ilivyotolewa taarifa awali na kisha kukanushwa jana?

Au kwa nini michezo hiyo isingerudishwa nyuma (kama inawezekana) ili wachezaji hao wazitumikie timu zao kisha kwenda kambini?

TFF imesahau kwamba maandalizi ya mchezo sio mazoezi tu, ni pamoja na utengenezaji wa mbinu na mifumo.

Ndio maana hata kwa wale wachezaji wanaocheza nje TFF inavitaarifu vilabu vyao ni lini wanawahitaji. Na ni lazima iwe mapema ili kumpa kocha muda wa kuwaandaa kimbinu kabla ya mchezo.

Timu kama Yanga mfano, inawakosa wachezaji wake watano mazoezini, halafu wachezaji hao wanaruhusiwa kuja kucheza siku ya mechi?

Je wataweza kufahamu na kutimiza maagizo waliyoelekezwa wenzao mazoezini ? jibu ni HAPANA.

Labda kama wataruhusiwa warejee kwenye vilabu vyao mapema siku mbili au hata tatu kabla ya mchezo ili wapate muda wa kufanya mazoezi ya mwisho na wenzao.

Lakini sio kuwaruhusu siku ya mchezo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’