Ilikuwaje Yanga ikawa hailipi kodi ya Jengo?

Yanga Damu By Yanga Damu
β€’
17 Aug 2017
Ilikuwaje Yanga ikawa hailipi kodi ya Jengo?
Kampuni ya Msolopa kupitia tangazo lake ililotoa kwenye Gazeti moja la Serikali leo, imetoa taarifa juu ya kuuzwa kupitia mnada majengo mbalimbali likiwemo la klabu ya Yanga kutokana na kudaiwa deni la zaidi ya Mil 300 na Wizara ya Ardhi.

Wizara ya Ardhi imetoa idhini kwa kampuni hiyo kuendesha mnada huo unaotarajiwa kufanyika Jumamosi, August 19.

Tunafahamu viongozi wamesema wanalishughulikia hili na tunaamini watafanikiwa kulipa deni hilo kwa wakati kama ilivyoamriwa na Mahakama kuepuka aibu hiyo ya mwaka.

Jambo la kujiuliza hapa, ilikuwaje klabu ya Yanga ikaacha kulipa hadi malimbikizo ya ada ya jengo na kiwanja kufikia Mil 300?

Ina maana kwa miaka mingi kodi hiyo ilikuwa hailipwi? Kweli viongozi walikuwa serious?

Hatuwezi kumlaumu MKwasa na viongozi wenzake wa sasa kwani tunaamini deni hilo ni la muda mrefu. Tunaunga mkono juhudi zao za kutaka kulipa deni hilo kulinusuru jengo la kihistoria la Klabu ya Yanga lisipotee.

Kuna ulazima kwa Yanga kubadili mfumo wake wa uendeshaji ,klabu iendeshwe kibiashara zaidi (KAMPUNI).

Ili kupitia mfumo huo waajiriwe watu ambao wanaweza kuwajibishwa wanapofanya makosa kupitia nyadhifa zao.

Mambo haya yametokea kwa sababu kuwa na mfumo mbovu pamoja na kukosekana uongozi thabiti, haiwezekani klabu kubwa kama Yanga ikatelekeza jengo lake ilihali inafahamu ni moja ya vitega uchumi vyake.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
24m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
49m ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
14h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’