Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi, Salum Umande Chama amesema tukio la kiungo wa Simba James Kotei kumpiga ngumi Gadiel Michael wakati wakiwania mpira litachunguzwa.
Mwenyekiti huyo wa moja ya Kamati za TFF amesema tukio hilo halikuchukuliwa hatua uwanjani na mwamuzi Jonesi Rukiyaa pengine kwa kuwa hakuliona.
Lakini hatua zinaweza kuchukuliwa baada ya Kamati husika kupitia mchezo huo na kujidhihirisha kuwa kosa lililofanyika linastahili adhabu.
Tukio hilo halitakuwa la kwanza kuchukuliwa hatua kwa mchezaji licha ya kuwa mwamuzi hakuona wakati wa mchezo.
Msimu uliopita Beki wa Yanga Kelvin Yondani alimtemea mate Asante Kwasi wa Simba na baadae Yondani alifungiwa michezo mitatu.
Pia adhabu iliwahi kutolewa kwa Juma Salamba, beki wa Majimaji aliyempiga kiwiko Emmanuel Martin msimu uliopita.
Hata Obrey Chirwa na Abdi Banda ambao sasa hawachezi soka Tanzania nao waliwahi kukumbwa na adhabu katika mazingira hayo

ADVERTISE HERE