Mfumo tuliotumia ndio uliwapa uhuru wa kucheza viungo wa Simba - Fei Toto

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
2 Oct 2018
Mfumo tuliotumia ndio uliwapa uhuru wa kucheza viungo wa Simba - Fei Toto
Kiungo wa Yanga, Feisal Salum 'Fei Toto' amesema, sababu kubwa iliyofanya Simba wang’are sehemu ya katikati inayochezwa na Mzambia Cletus Chama, Mghana James Kotei na Jonas Mkude katika mchezo wao ni maagizo waliyopewa na kocha wao, Mwinyi Zahera.

Safu ya kiungo ya Simba iliyoundwa na wachezaji hao, iliwapoteza kabisa wale wa Yanga kama Mkongo Papy Tshishimbi na Fei Toto katika eneo hilo la katikati.

Fei Toto amesema, hawakuhofia viungo wa Simba, lakini walicheza kwa maelekezo waliyopewa na mwalimu wao.

"Mwalimu alihitaji sisi tukabe kuliko kushambulia, mfumo wake ndio ulitaka hivyo lakini kama angetuambia tucheze tungefanya hivyo na kuacha kujilinda," alisema Fei Toto.

Aliongeza kwa kusema, licha ya kukaba, walikutana na changamoto kubwa kutoka kwa viungo wa Simba ndani ya dakika 90 katika mchezo huo.

"Wenzetu walikuwa wengi kwenye kiungo kwa hiyo ikafanya mchezo kuwa mgumu kwetu na kuzuia muda wote lakini juhudi zetu tulizionyesha katika kipindi chote," alisema kiungo huo maarufu Yanga.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →