Nyota Paul Godfrey 'Boxer' na Abdallah Shaibu 'Ninja' jana waligeuka mwiba kwa safu ya ushambuliaji ya Simba baada ya kucheza jino kwa jino na washambuliaji hao.
Godfrey 'Boxer' ambaye ndio mchezo wake wa kwanza kwa watani wa jadi, alionyesha ukakamavu katika safu ya ulinzi Yanga.
Beki huyo aliweza kutembea hatua kwa hatua na Mohammed Hussein 'Tshabalala', ambaye alikuwa anatumika katika upande wa kushoto kupeleka mashambulizi, hali ambayo iliwafanya Simba waanze kupitia upande wa kulia kwa Shomari Kapombe.
Wakati huohuo Ninja aliweza kumtuliza Emmanuel Okwi ambaye katika pambano hilo alikuwa akicheza kwa kuvizia wakati huo huo kwa upande wa Kagere, Ninja alikuwa akitumia nguvu zake kumzuia mchezaji huyo ambaye alikuwa anatumia nguvu na akili kwa pamoja katika kupeleka mashambulizi.
Hata hivyo Simba waliweza kutawala katika upande wa kiungo, sehemu ambayo Cletus Chama, James Kotei na Jonas Mkude waliitawala katika mchezo huo.
Yanga ilicheza kwa kujihami zaidi na kufanikiwa kuondoka na alama moja muhimu iliyofanywa wafikishe alama 13 na kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

ADVERTISE HERE