FT : Simba 0-0 Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Sep 2018
FT : Simba 0-0 Yanga
Mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara kati ya Simba dhidi ya Yanga uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa Jumapili jioni umemalizika kwa suluhu ya bila kufungana.

Simba ilitawala mchezo huo kwa muda mwingi lakini uimara wa safu ya ulinzi ya Yanga hasa mlinda lango Beno Kakolanya ulifanikisha kuondoka alama moja muhimu.



Kocha ya Yanga Mwinyi Zahera alitambua ugumu wa mchezo leo hivyo akaamua kutilia mkazo zaidi kwenye safu ya ulinzi kwa kumuanzisha Abdallah Shaibu Ninja kama kiungo mkabaji hivyo kufanya Yanga iwe na walinzi watatu nyuma.

Kwa kiasi kikubwa mbinu hiyo iliiwezesha Yanga kuweza kuwadhibiti kabisa washambuliaji wa Simba.







Beki Andrew Vicent Chikupe aliweza kumdhibiti ipasavyo Meddie Kagere anayetegemewa na Simba kwenye kupachika mabao.

Nafasi pekee ya wazi kwa upande wa Yanga ilipotezwa na kiungo Papi Tshishimbi mapema kwenye kipindi cha pili baada ya shuti lake kupaa juu ya lango.

Yanga imeendeleza rekodi ya kutopoteza msimu huu ikiwa na alama 13 baada ya kushuka dimbani mara tano.

Simba imeshuka dimbani mara sita na imetimiza alama 11 baada ya matokeo ya mchezo wa leo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’