Yanga hii kila mchezaji anafunga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Sep 2018
Yanga hii kila mchezaji anafunga
Tofauti na Simba ambayo imekuwa ikiwategemea Meddie Kagere na John Bocco katika kuzifumania nyavu, Yanga imedhihirisha kila mchezaji anaweza kufunga.

Kagere na Bocco ndio waliofunga mabao sita ya Simba mpaka sasa wakati mabao ya Yanga yamefungwa na wachezaji saba tofauti.

Heritier Makambo, Amissi Tambwe, Mrisho Ngasa, Deus Kaseke, Ibrahim Ajib, Andrew Vicent na Kelvin Yondani wamefunga mabao tisa ya Yanga.

Kwa takwimu hizi, Yanga inahitaji kumdhibiti Kagere kwenye mchezo wa leo baada ya Bocco kukosekana kutokana na kutumikia adhabu ya kadi nyekundu.

Wachezaji wengine ambao itafaa wachungwe na safu ya ulinzi ya Yanga ni pamoja na Emmanuel Okwi na Shiza Kichuya.

Kichuya amekuwa na 'BAHATI' ya kufunga kwenye michezo ya watani wa jadi akiwa amefunga mabao matatu.

Hakuna wasiwasi upande wa safu ya kiungo kwani Tshishimbi, Fei Toto na Ajib wanao uwezo kuwafunika viungo wa Simba.

Kwa mfumo anaotumia kocha Mwinyi Zahera Yanga itakuwa na idadi kubwa ya wachezaji kwenye sehemu ya kiungo kwani washambuliaji wote wa pembeni watakuwa na majukumu katika nafasi hiyo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
1h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
2h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
5h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’