Kila la kheri Yanga, kila la kheri mabingwa wa kihistoria

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Sep 2018
Kila la kheri Yanga, kila la kheri mabingwa wa kihistoria
Leo Jumapili saa 11 jioni Yanga itakuwa uwanja wa Taifa kupepetana na watani zao wa jadi Simba kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara.

Yanga iliweka kambi mkoani Morogoro mwanzoni mwa wiki hii na ilirejea jijini Dar es salaam juzi, siku mbili kabla ya mchezo.

Kambi hiyo ilikuwa maalum kwa ajili ya maandalizi kuelekea mchezo huo wenye 'hadhi' zaidi kuliko michezo mingine ya ligi kwa kuwa unazikutanisha timu zenye historia ya aina yake.

Yanga ina matumaini makubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo kutokana na ubora wa kikosi chake msimu huu.

Ushindi wa michezo yote minne ya ligi umeongeza ari na kujiamini kwa kikosi cha Yanga.

Kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera amesema vijana wake hawana hofu yoyote kuikabili Simba leo kwani wamefanya maandalizi ya kutosha.

Zahera anaamini Simba ndio itakuwa na wakati mgumu wa kukabiliana na Yanga ambao iko kwenye kiwango bora ikiwa imeshinda michezo yake yote ya ligi.

Kikosi cha Yanga huenda kisiwe na mabadiliko makubwa.

Beno Kakolanya, Paul Godfrey (Boxer), Gadiel Michael, Andrew Vicent, Kelvin Yondani, Papi Tshishimbi, Mrisho Ngasa, Feisal Salum, Heritier Makambo, Ibrahim Ajib na Deus Kaseke ndicho kikosi ambacho huenda kikashuka dimbani leo.

Nahodha wa Yanga Kelvin Yondani amewataka mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanja wa Taifa kushuhudia 'mziki mnene' wa mabingwa hao wa kihistoria Tanzania.

Tiketi zimeendelea kuuzwa kwa kasi ambapo mpaka sasa taarifa zilizotolewa ni kuwa Tiketi za VIP A tayari zimeuzwa zote.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’