Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema vijana wake wako tayari kwa mchezo wa keshokutwa Jumapili dhidi ya Simba.
Zahera amesema Yanga itaingia kwenye mchezo huo bila ya kuwa na presha yoyote hasa ikizingatiwa imeshinda michezo yake yote minne ya mwanzo kwenye ligi kuu ya Tanzania bara.
"Hatuna wasiwasi, vijana wako tayari kwa mchezo. Ushindi tuliopata kwenye michezo minne ya kwanza umeongeza kujiamini kwa wachezaji wetu," amesema Zahera.
"Pia Kambi tuliyoweka mkoani Morogoro imekuwa na mafanikio kwetu. Tuna matumaini makubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa keshokuta"
Naye Meneja wa Yanga Nadir Haroub amesema wachezaji wote waliokuwa kambini mkoani Morogoro wana ari kubwa ya kuibuka na ushindi mchezo wa keshokutwa.
Amesema hakuna majeruhi wengine zaidi ya Juma Abdul na Juma Mahadhi ambao hawakujumuishwa kwenye kambi ya mkoani Morogoro.

ADVERTISE HERE