Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Emmanuel Amunike leo ametangaza majina 30 ya wachezaji wanaounda kikosi cha timu ya Taifa kitakachoingia kambini kujiandaa na michezo miwili ya kusaka tiketi ya kufuzu fainali za AFCON 2019 dhidi ya Cape Verde.
Katika orodha hiyo amekosekana kiungo Ibrahim Ajib fundi wa mpira huku Yanga ikirejesha wachezaji wake wote waliokuwa wameitwa awamu iliyopita.
Wachezaji hao ni mlinda lango Beno Kakolanya, walinzi Andrew Vicent, Kelvin Yondani na Gadiel Michael. Bila kumsahau kiungo Feisal Salum 'Fei Toto'
Kukosekana kwa Ajib kwenye kikosi hicho kumewashangaza wengi hasa ikizingatiwa kiungo huyo amekuwa kwenye kiwango bora kabisa tangu kuanza kwa msimu huu.
Akiwa amecheza michezo minne kwenye ligi kuu ya Tanzania Bara, Ajib ametengeneza mabao matano lakini pia akiwa amefunga bao moja.
Stars inatarajiwa kumenyana na Cape Verde kwenye mchezo wa kwanza ugenini October 12 kabla ya kurudiana siku nne baadae October 16 kwenye uwanja wa Taifa.
Kama Stars itashinda michezo hiyo basi itakuwa imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu kwa fainali za michuano ya AFCON itakayofanyika mwezi Juni 2019 nchini Cameroon.

ADVERTISE HERE