Thabani Scara Kamusoko ni mmoja wa viungo waliojijengea heshima ya kipekee katika klabu ya Yanga.
Tangu alipotua Yanga miaka mitatu iliyopita, Kamusoko alikuwa mmoja wa wachezaji wa kutumainiwa wa kikosi cha kwanza lakini kuanzia msimu uliopita mambo yalibadilika.
Msimu wa 2017/18 haukuwa mazuri kabisa kwa kiungo huyo Maestro ambaye alisumbuliwa na majeraha ya goti yaliyomyima fursa ya kuitumikia Yanga kwenye michezo mingi.
Tangu kuwasili kwa kocha Mwinyi Zahera, Kamusoko amekuwa hapati nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga, ikielezwa bado hajaweza kuimarika kikamilifu kutoka kwenye majeraha yanayomsumbua.
Yanga ikiwa tayari imecheza michezo minne ya ligi msimu huu, Kamusoko bado hajafanikiwa kupenya kwenye kikosi cha Zahera anayependelea kuwatumia viungo Papi Tshishimbi na Feisal Salum.
Hata hivyo kiungo huyo amebainisha kuwa yuko karibu kabisa kurejea kikosini baada ya kuendelea kuimarika kwa afya yake.

ADVERTISE HERE